Mshindi wa Pili BBA 2014, Tayo Faniran azidi kufanyiwa mambo makubwa
Tayo Faniran ni jina lililovuma sana katika jumba la Kaka Mkubwa 'Big Brother' Africa 2014. Licha kwamba alikuwa na kaumaarufu fulani kikwaokwao lakini kwa nchi zingine tumemjua kupitia BBA 2014. Ndio, alikuwa hajulikani kwetu. Alikuwa ni mshiriki kutoka Nigeria, mtu mwenye misimamo, mcheshi pia very social kwa kipindi chote alichokuwa BBA.Tayo mwisho wa siku alifanikiwa kuwa mshindi wa pili katika safari ya BBA, na mshindi wa Kwanza alikuwa kaka yetu wa Ukaye, Idris Sultan ambapo alijinyakulia kitita cha dola za kimarekani laki tatu ($300,000).
Lakini Tayo ameweza kufanyiwa mambo makubwa na mashabiki wake ukilinganisha na mshindi wa kwanza. kitu cha kwanza kabisa baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili, Milionea wa Nigeria Ayiri Emami ametangaza kumpatia Tayo dola za kimarekani laki tatu na hamsini ($350,000) ikiwa imezipita hadi zile za mshindi wa kwanza. Pia jana tarehe 20/12/2014 amefanyiwa party kubwa ya kukaribishwa nyumbani akitokea South Africa alikokuwa anafanya reality show kwa kipindi chote baada ya BBA.
Mbali na hilo jamaa wanajiita @malivelihood wamemfanyia customization ya limited edition ya Iphone 6. Kwaujumla jamaa katisha sana.

0 comments :
Post a Comment