Breaking News
Loading...
Thursday, December 18, 2014

Bird Man amjibu Lil Wayne juu ya Kujitoa Young Money Records

Majuzi Lil Wayne alionesha nia yake ya kutaka kuchomoka kwenye record label ya Young Money kupitia mitandao ya Twitter. Moja ya post zake ni hii ambayo alisema '"I want off this label and nothing to do with these people." Akimaanisha kuwa 'nataka kuchomoka kutoka hii label na kuachana na hawa watu'. Hii ishu ya Lil Wayne 'Wizzy'  imekuja baada ya kuona mabosi wake hao wanaichelewesha kwa makusudi albamu yake mpya.

Lakini katika kulijibu hilo, Bosi wa Young Money Cash Money, Bird Man amefunguka na kusema kuwa Lil Wayne hawezi kutoka hiyo label kwani mkataba ulishafungwa so ni ngumu kwake kuchomoka. Amedai kuwa Wizzy anawaza muziki wakati yeye anawaza biashara, hivyo ataitoa albam hiyo muda wowote akiona kibiashara unafaa na sio kama Wizzy anavyotaka.
 
Lil Wayne kwasasa anajiona kama mfungwa vile ndani ya Young Money Record Label.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top